Ruka hadi maudhui
Anza na Lishe
Shajara
Milo
Ushauri
Wasifu
Orodha ya manunuzi ya kisukari
Vyakula 38 vinavyotumika kwenye mpango wa milo. Weka alama unavyonunua.
Chapisha au hifadhi PDF
0 kati ya 38
Vyakula vya wanga
Unga wa dona
Unga wa mahindi yasiyokobolewa. Una nyuzinyuzi zinazopunguza kasi ya kupanda kwa sukari.
Ndizi za kupika
Chemsha au pika kwenye mchemsho. Ndizi 1–2 kwa mlo.
Magimbi
Chemsha. Gimbi moja ukubwa wa kiganja linatosha.
Viazi vitamu
Chemsha au choma pamoja na ganda. Kipande ukubwa wa nusu kiganja.
Mihogo
Chemsha. Kula kiasi kidogo pamoja na mboga na protini.
Mchele wa brown
Una nyuzinyuzi zaidi kuliko mchele mweupe. Kikombe ½–1.
Mahindi mazima
Kwa makande pamoja na maharage na mboga.
Protini
Mayai
Chemsha. Yai moja kwa kifungua kinywa.
Nyama
Chagua isiyo na mafuta mengi. Vipande 3 ukubwa wa kiberiti.
Samaki
Chemsha au oka. Kipande ukubwa wa kiganja.
Dagaa
Protini na kalsiamu kwa bei nafuu. Kikombe ½–1.
Kuku
Kwa supu au kuchemsha. Ondoa ngozi.
Maharage
Protini na nyuzinyuzi. Kikombe ½ kwa mlo.
Njegere
Pika pamoja na wali wa brown na karoti.
Karanga na mbegu
Karanga
Kiganja kimoja ni asusa nzuri.
Korosho
Punje 10 kama asusa.
Mbegu za maboga
Kiganja kimoja kama asusa.
Mboga
Mboga za majani
Mchicha, sukuma wiki, matembele, kisamvu na nyingine. Vikombe 1–2 kila mlo.
Bamia
Kwa mboga au maji ya bamia ya alfajiri.
Tango
Asusa nzuri isiyopandisha sukari.
Nyanya chungu
Kikombe kimoja pamoja na mlo wa usiku.
Beetroot
Kwa juisi pamoja na karoti na apple.
Matunda
Parachichi
Mafuta mazuri. Nusu parachichi kwa asusa.
Chungwa
Chungwa moja kama asusa.
Zabibu
Punje 10–15 kwa asusa.
Pera
Tunda lenye vitamini C na nyuzinyuzi.
Ubuyu
Tumia ubuyu wa asili kwa juisi, si pipi za ubuyu zenye sukari.
Apple
Kwa juisi ya mboga na matunda bila sukari.
Maziwa
Mtindi
Chagua usio na sukari.
Maziwa
Kunywa bila sukari; ongeza viungo kwa ladha.
Viungo
Mdalasini
Kwa maji ya alfajiri, chai na maziwa.
Mchaichai
Kwa chai ya viungo bila sukari.
Tangawizi
Kwa chai, juisi na maji ya viungo.
Vitunguu saumu
Punje 3 dakika 45 kabla ya kulala, kama ilivyo kwenye mpango.
Karafuu
Kwa maji ya karafuu na mdalasini.
Manjano
Kwa maji ya alfajiri na maziwa ya viungo.
Iliki
Kwa chai ya viungo.
Vingine
Olive oil
Kijiko kimoja kikubwa kwenye juisi au saladi.
Shajara
Milo
Ushauri
Wasifu